Mwanariadha Mkongwe Aliyeweka Historia ya Kimataifa

John Steven Akhwari anakumbukwa katika ulimwengu wa michezo hususani ile ya Olympic. Alishiriki katika mchezo wa riadha akiiwakilisha Tanzania katika michezo ya Olympic iliyofanyika nchini Mexico mwaka 1968.

Wakati wa mashindano,Akhwari alianguka na kuumia vibaya gotini. Madaktari walimwendea na kumfunga bandeji huku wakidhani kwamba mwanariadha huyo ndio amefikia mwisho wa mashindano na atajitoa. Mambo yalikua tofauti. Akhwari akasimama na kuendelea kukimbia. Kitendo hicho kiliwashangaza wauguzi na mashabiki. Aliendelea kukimbia hivyo hivyo akiwa na maumivu makali bila kujali kwamba alikua ameumia vibaya mguu wake wa kulia hadi kupelekea mshangao mkubwa sana kwa watu katika mji ule kwa ile siku. Hakushinda mashindano hayo lakini ikafanya mshindi wa siku Mamo Wolde wa Ethiopia asiwe stori kubwa bali Mtanzania huyu ndie aliyekuwa stori kwa vyombo vya habari vya mji ule na vingine vikubwa duniani.

Kama watanzania tunajifunza kutoka kwake kuwa na uzalendo wa nchi yetu. Waandishi wa habari mbalimbali walipomfuata Akhwari na kumuuliza ni kwa nini aliamua kukimbia licha ya kuwa aliumia sana akajibu "My country did not send me 5,000 miles to start the race; they sent me 5,000 miles to finish the race," yaani nchi yangu haikunituma maili 5,000 kuanza mbio, walinituma maili 5,000 kumaliza mbio.

Akhwari ameishi kwa miaka mingi kijijini na mke wake pamoja na watoto wao sita. Alizaliwa mwaka 1938 Mbulu. Ni mkulima anayefanya kazi kwa bidii sana. Kwa mara moja moja dunia imekua ikimkumbuka sana na kuweka baadhi ya ishara za kumkumbuka. Alitunukiwa medali ya ushujaa wa nchi mnamo mwaka 1983.Aliruhusu jina lake litumike katika chuo cha mafunzo ya wanariadha wanaoshiriki mashindano ya Olympic hapa nchini Tanzania. Alialikwa kwenye mashindano ya Olympic ya mwaka 2000 nchini Sydney Australia. Baadaye alionekana Beijing China kama balozi anayejali katika maandalizi ya Olympic mwaka 2008. Yeye ndiye aliyebeba mwenge wa Uhuru na kuongoza mbio za mwenge jijini Dar es salaam mwezi April 13,2008.

Share this article

About Author

Super User
Login to post comments

Visitors Counter

027827
Today
Yesterday
This Week
Last Week
This Month
Last Month
All days
45
129
649
26031
4717
4022
27827
Your IP: 50.19.34.255
2018-02-24 14:22

The Lastest posts

Contact Us

  • Tanzania Book of Records
  • Sinza Mori, T-Garden street,
  • House No 13
  • P.O.BOX 62279 Dar es salaam
  • 0737208872

       > Site Administrator

Our Facebook Page