Msanii Mkongwe wa Nyimbo za Taarabu

Fatuma binti Baraka maarufu kama Bi Kidude ni msanii mkongwe na mahiri sana katika fani ya muziki wa mwambao ambao hujulikana kwa jina la taarabu. Muziki huu ambao ni mchanganyiko wa wa muziki kutoka nchi za kiarabu na vionjo vya muziki wa kiafrika umekita sana katika mwambao wa Afrika Mashariki yaani Zanzibar, Lamu, Mombasa na kwingineko.Bi Kidude  alifariki mwaka 2013 huko Bububu visiwani Zanzibar. Mwaka aliozaliwa haujulikani ila alikisiwa kuwa na miaka 102, alizaliwa katika kijiji cha Mfagimarigo Zanzibar katika familia ya watoto saba.Baba yake alikuwa mfanyabiashara wa nazi zao ambalo ni la kutumainiwa sana Zanzibar. Bi Kidude hakufahamu tarehe halisi aliyozaliwa.Alichojua na kwamba alizaliwa kipindi rupia ikitumika kama fedha na alikua na uhakika ni kabla ya vita vya kwanza vya dunia.Wataalamu wa mahesabu walipiga hesabu baada ya kupata taarifa hizo na kumkabidhi miaka yake kuwa ni zaidi ya miaka 90.

Bi Kidude anasema alijifunza uimbaji kutoka kwa msanii mkongwe aliyetamba sana enzi hizo Sitti binti Saad akiwa na umri wa miaka kumi.Wageni kutoka sehemu mbalimbali walikuwa wakifika Zanzibar kumwona Sitti. Bi Kidude na Sitti walikuwa wako karibu,Bi Kidude alikuwa akiwapeleka wageni wale nyumbani kwa Bi Sitti ambapo bi Sitti alikuwa akiwaimbia wale wageni na yeye huku nje alikuwa akimsikiliza kwa makini na kumfuatiza jinsi alivyokuwa akiimba. Aliendelea hivyo hadi akawa mahiri sana katika uimbaji.

Bi Kidude alitoroka nyumbani kwao Zanzibar alipokuwa na miaka 13 na kukimbilia Tanzania Bara baada ya kulazimishwa kuolewa. Alipokuwa kigoli wa kutosha kuolewa, aliolewa ingawa ndoa hiyo haikudumu kutokana na manyanyaso aliyokua akiyapata, hivyo aliamua kukimbilia Misri ikiwa ni miaka ya 1930,huko aling'ara sana katika fani yake ya uimbaji na uchezaji ngoma.Miaka ya 1940 aliamua kurudi nyumbani Zanzibar ambapo aliendelea na shughuli zake za uimbaji.

Mbali na uimbaji Bi Kidude alikuwa anajishughulisha na biashara ya wanja na hina ambavyo alikuwa anavitengeneza yeye mwenyewe, pia alikuwa mtaalamu wa matibabu kwa dawa za mitishamba na alikuwa mwalimu wa Unyago, na kati ya wanafunzi aliowahi kuwawapa mafunzo ya unyago hakuna aliyewahi kupata talaka.Bi Kidude hakuweza kufanikiwa kuwa na ndoa iliyodumu pamoja na kuwa mwalimu mzuri katika mambo ya unyago na kuwafundisha mabinti namna ya kuishi na waume zao, kwani hadi mauti inamfika hakuwa anaishi na mume.

Bi Kidude alikulia katika mazingira na utamaduni awa kiarabu ambapo mwanamke anatakiwa wakati wote akiwa hadharani ajifunike lakini aliona kwamba ni sheria za kitamaduni kutoka Uarabuni hivyo aliamua kuondoa hijabu mwilni mwake, akavaa kama Mtanzania.Aliendelea kuvunja miiko mingine kwa kunywa pombe na kuvuta sigara jambo ambalo si la kawaida kwa wanawake wa Zanzibar.

Katika nchi alizowahi kutembelea ni pamoja na Oman,Hispania,Ujerumani,Uingereza na Ufuransa.Alipata tuzo mbalimbali ambazo ni pamoja na ile ya Tamasha la Filamu la Nchi za Jahazi (ZIFF) mwaka 1999 tuzo za maisha na mwaka 2005 tuzo za WOMAX ilienda kwake. Nyimbo alizowahi kuimba ni pamoja na Muhogo wa Jang'ome, Sikitiko, Juhudi za Wasiojiweza, Kijiti, Jua Toka, Ukichukua, Ya Laiti na alikuwa akiimba kiswahili na kiarabu. Hakuwahi kupata elimu nyingine zaindi ya Kurani.

Wanamuziki wengi hapa nchini na watanzania kwa ujumla wanajivunia kuwa na mtu kama huyu aliyeweza kuonyesha uwezo wa kipaji chake kwa kuimba hadi akiwa mzee wa miaka mia na moja jambo ambalo wanamuziki wachache hapa duniani wamewahi kufanya hivyo. "Ya laiti" ni wimbo aliouimba miaka michache kabla ya kifo chake.

Share this article

About Author

Super User
Login to post comments

Visitors Counter

027824
Today
Yesterday
This Week
Last Week
This Month
Last Month
All days
42
129
646
26031
4714
4022
27824
Your IP: 50.19.34.255
2018-02-24 14:21

The Lastest posts

Contact Us

  • Tanzania Book of Records
  • Sinza Mori, T-Garden street,
  • House No 13
  • P.O.BOX 62279 Dar es salaam
  • 0737208872

       > Site Administrator

Our Facebook Page