MAKAMU WA RAIS ALIYEONGOZA KWA MUDA MREFU

Mheshimiwa Mfaume Rashid kawawa ni Makamu wa Rais wa Tanzania aliyeongoza kwa muda mrefu tangu mwaka 1964 hadi 1977. Jumla ya kipindi chake alichoongoza kama Makamu wa Rais ni miaka 13 ambayo haijawahi kufikiwa na Makamu Rais yoyote wa awali au wengine waliomfuatia baada ya kustaafu. Hii imefanya kutambulika kama Makamu wa Rais aliyeongoza kwa muda mrefu zaidi katika historia ya Tanzania.

Kawawa alizaliwa Mei 27, 1926 katika kijiji cha Matepwende wilaya ya  Songea, Tanganyika  kwa sasa inajulikana kama Tanzania.Baada ya kumaliza elimu ya msingi alipata elimu ya sekondari katika shule ya serikali ya Tabora  (Tabora Government Secondary School )aliyosoma mwalimu Julius Kambarage  Nyerere kiongozi aliyepigania uhuru wa Tanganyika,  Baada ya kustaafu kwake Kawawa alibakia nyuma ya pazia katika ushawishi wa siasa. Alifariki Desemba 31, 2009  Dar es Salaam akiwa na umri wa miaka 83. 

Rashid Kawawa alitumikia katika ofisi kadhaa za kisiasa  Tanganyika na baadaye Tanzania kwa karibu nusu karne kama ifuatavyo:

Mwaka 1960, aliteuliwa kuwa Makamu wa Rais wa TANU,

Kati ya Januari 22, 1962 na Desemba 9, 1962, Rashid Kawawa alikuwa Waziri Mkuu wa Tanganyika,

Desemba 9, 1962 Tanganyika ikawa jamuhuri na Rashid Kawawa aliteuliwa  kuwa  Makamu wa kwanza wa Rais wa Jamhuri ya Tanganyika,

 Mwaka 1964 baada ya Muungano wa Tanganyika na Zanzibar (Tanzania) , Kawawa aliteuliwa kuwa  Makamu wa pili wa Rais wa Tanzania na kuwa  msaidizi  mkuu wa Nyerere  katika  masuala ya bara na kama kiongozi wa Bunge.

Rashid Kawawa alikuwa pia Mbunge katika Bunge la Tanganyika na Tanzania kwa miaka mingi.

Rashid Kawawa alijitoa serikalini mwaka 1985 na mwaka 1994 alitangaza kustaafu siasa. 

Mwaka 1994, alitangaza kustaafu kwenye siasa.

Alipokuwa Waziri Mkuu na Makamu wa Rais, Rashid Kawawa alihimiza  kukuzwa kwa Kiswahili kama njia mojawapo ya mawasiliano nchini Tanzania. Hii imesaidia kuungana zaidi ya makundi 120 ya kikabila. Mapema baada ya uhuru kama Waziri Mkuu, Rashid Kawawa, alitangaza  Kiswahili  kuwa lugha ya taifa kutumiwa katika kazi za serikali na umma na pia  katika Bunge  na Kiingereza kuwa lugha ya pili

Mwaka 2007 Rashid Kawawa  alitambuliwa na Chuo Kikuu cha Massachusetts Dartmouth  kama mpiganaji mkubwa  wa uhuru, usawa na haki barani Afrika. Alitunukiwa tuzo ya  Drum Major Award, tuzo ya kumbukumbu ya urithi wa Dk Martin Luther King Jr. - anayejulikana  kama  mmarekani mweusi  mpiganaji  wa usawa na haki nchini Marekani.

Share this article

About Author

Super User
Login to post comments

Visitors Counter

027821
Today
Yesterday
This Week
Last Week
This Month
Last Month
All days
39
129
643
26031
4711
4022
27821
Your IP: 50.19.34.255
2018-02-24 14:21

The Lastest posts

Contact Us

  • Tanzania Book of Records
  • Sinza Mori, T-Garden street,
  • House No 13
  • P.O.BOX 62279 Dar es salaam
  • 0737208872

       > Site Administrator

Our Facebook Page