MAKAMU WA RAIS WA KWANZA WA ZANZIBAR

Kwa mara ya kwanza katika historia ya Tanzania Mhe. Maalim Seif Sharif Hamad alichaguliwa kuwa Makamu wa Rais wa Zanzibar mwaka 2010 hadi 2015 .Maalim Seif Hamad anajulikana kama katibu mkuu wa chama cha upinzani cha Civic United Front (CUF)  na Makamu wa kwanza wa Rais wa Zanzibar. 

Alizaliwa  Oktoba 22, 1943 katika kijiji  cha Nyali, Mtapwe  Pemba.Hamad alipata elimu ya msingi  katika  shule ya msingi Uondwe na shule ya wavulana Wete, Pemba mwaka 1950-1957 . Aliendelea na elimu  ya Sekondari  katika Shule ya Sekondari ya  King George VI Memorial,  Zanzibar Town mwaka 1958-1961. Hamad alihudhuria elimu ya kidato cha tano na sita  katika shule hiyo hiyo  mwaka 1962-1963.

Baada ya kumaliza elimu ya sekondari  Desemba  1963, kwa kipindi cha miaka tisa (1964-1972) alizuiwa kujiunga na elimu ya juu ya chuo kikuu kwa sababu alikuwa miongoni mwa watu waliotakiwa kujaza moja ya nafasi za kazi katika utumishi wa umma uliosababishwa na kuondoka kwa wingi wa maofisa wa Uingereza mwaka 1964 baada ya kutakiwa kufanya hivyo na serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar.Alipewa nafasi ya kufundisha katika shule za sekondari  kabla ya kujiunga na Chuo Kikuu cha Dar es Salaam mwaka 1972-1975, na kufuzu vizuri katika Stashahada ya Sayansi ya Siasa, Utawala wa Umma na Uhusiano wa Kimataifa.

Mwaka  1977-1980 Hamad alikua Mbunge wa Baraza la Mapinduzi  Zanzibar na  Waziri wa Elimu , mwanachama mwanzilishi wa Baraza la Wawakilishi Zanzibar ( 1980-1989 ) na Mbunge wa Tanzania (1977) , Mjumbe wa Kamati Kuu na Halmashauri Kuu ya Taifa ya Chama cha Mapinduzi (CCM) -  Chama Tawala cha Tanzania mwaka  ( 1977-1987 ) , Mkuu wa Kiuchumi na Idara ya Mipango ya CCM ( 1982-1987 ) na Waziri Kiongozi wa Zanzibar (6 February 1984-22 Januari 1988) Baada ya migogoro na viongozi wa Chama cha Mapinduzi (CCM) alifukuzwa kutoka chama hicho. Januari 1988 alitolewa kutoka Baraza la Mapinduzi na kama Waziri Kiongozi wa Zanzibar. Mei 1989 alikamatwa na kufikishwa mahakamani kwa  madai ya kisiasa na kudaiwa kukutwa na nyaraka za siri za serikali. Mwaka 1989-1991 Alifungwa katika  gereza kuu la Zanzibar kama mfungwa wa dhamiri.

Tanzania ilipopitisha mfumo wa vyama vingi vya siasa mwaka 1992, Hamad pamoja na wanachama wengine wa zamani wa CCM walianzisha chama cha CUF (Civic United Front) . Uchaguzi wa kwanza wa vyama vingi ulifanyika mwaka 1995 na Maalim Seif  Hamad alikuwa mgombea Urais wa Zanzibar kupitia  chama cha CUF. Mgombea wa CCM Salmin Amour alishinda uchaguzi kwa kumpita kwa kura chache Maalim. Waangalizi walibainisha dosari kubwa katika uchaguzi huo na wanachama wa CUF hawakukubaliana na matokeo kwa madai ya kuibiwa kura.

Katika uchaguzi wa mwaka 2000 Maalim Seif Hamad aligombea tena Urais wa Zanzibar kupitia chama cha CUF na  kushindwa tena  na mgombea wa CCM Amani Abeid Karume  . Timu ya Jumuiya ya Madola ilieleza uchaguzi huo kama  ‘umesambaratika '

Aprili  2000, alikamatwa na kushtakiwa kwa madai ya  kushambulia kikosi cha polisi na kuiba silaha, Novemba 2003 Mahakama  ya Hakimu Mkazi Zanzibar walitupilia mbali mashtaka hayo.Katika uchaguzi wa mwaka 2005,kwa mujibu wa matokeo rasmi, Hamad alishindwa tena uchaguzi na Mgombea wa CCM Amani Abeid Karume ambaye alitangazwa mshindi wa Urais. CUF walikataa kumtambua Karume kama Rais. Waangalizi wa kimataifa, kama vile Jumuiya ya Madola, na National Democratic Institute  walibainisha wasiwasi mkubwa wa uadilifu wa uchaguzi huo, na Marekani kugomea sherehe za kuapishwa Kwa Abeid Karume kama Rais.

Tarehe 31 Oktoba 2010, Watanzania walipiga kura kumchagua Rais wa Tanzania na Zanzibar na Hamad aligombea, pamoja na Dk Ali Mohamed Shein wa chama tawala CCM ambaye alitangazwa kuwa mshindi  Novemba 2010.Hamadi alitangazwa kuwa  Makamu wa Rais wa kwanza Zanzibar wakati Dk Shein aliapishwa kama Rais mpya wa Zanzibar.

Share this article

About Author

Super User
Login to post comments

Visitors Counter

027826
Today
Yesterday
This Week
Last Week
This Month
Last Month
All days
44
129
648
26031
4716
4022
27826
Your IP: 50.19.34.255
2018-02-24 14:22

The Lastest posts

Contact Us

  • Tanzania Book of Records
  • Sinza Mori, T-Garden street,
  • House No 13
  • P.O.BOX 62279 Dar es salaam
  • 0737208872

       > Site Administrator

Our Facebook Page