John Steven Akhwari anakumbukwa katika ulimwengu wa michezo hususani ile ya Olympic. Alishiriki katika mchezo wa riadha akiiwakilisha Tanzania katika michezo ya Olympic iliyofanyika nchini Mexico mwaka 1968.

Wakati wa mashindano,Akhwari alianguka na kuumia vibaya gotini. Madaktari walimwendea na kumfunga bandeji huku wakidhani kwamba mwanariadha huyo ndio amefikia mwisho wa mashindano na atajitoa. Mambo yalikua tofauti. Akhwari akasimama na kuendelea kukimbia. Kitendo hicho kiliwashangaza wauguzi na mashabiki. Aliendelea kukimbia hivyo hivyo akiwa na maumivu makali bila kujali kwamba alikua ameumia vibaya mguu wake wa kulia hadi kupelekea mshangao mkubwa sana kwa watu katika mji ule kwa ile siku. Hakushinda mashindano hayo lakini ikafanya mshindi wa siku Mamo Wolde wa Ethiopia asiwe stori kubwa bali Mtanzania huyu ndie aliyekuwa stori kwa vyombo vya habari vya mji ule na vingine vikubwa duniani.

Kama watanzania tunajifunza kutoka kwake kuwa na uzalendo wa nchi yetu. Waandishi wa habari mbalimbali walipomfuata Akhwari na kumuuliza ni kwa nini aliamua kukimbia licha ya kuwa aliumia sana akajibu "My country did not send me 5,000 miles to start the race; they sent me 5,000 miles to finish the race," yaani nchi yangu haikunituma maili 5,000 kuanza mbio, walinituma maili 5,000 kumaliza mbio.

Akhwari ameishi kwa miaka mingi kijijini na mke wake pamoja na watoto wao sita. Alizaliwa mwaka 1938 Mbulu. Ni mkulima anayefanya kazi kwa bidii sana. Kwa mara moja moja dunia imekua ikimkumbuka sana na kuweka baadhi ya ishara za kumkumbuka. Alitunukiwa medali ya ushujaa wa nchi mnamo mwaka 1983.Aliruhusu jina lake litumike katika chuo cha mafunzo ya wanariadha wanaoshiriki mashindano ya Olympic hapa nchini Tanzania. Alialikwa kwenye mashindano ya Olympic ya mwaka 2000 nchini Sydney Australia. Baadaye alionekana Beijing China kama balozi anayejali katika maandalizi ya Olympic mwaka 2008. Yeye ndiye aliyebeba mwenge wa Uhuru na kuongoza mbio za mwenge jijini Dar es salaam mwezi April 13,2008.

Mtanzania apata medali ya shaba katika mchezo wa kutupa mkuki:

Mtanzania Shururwai Laanyuni amepata ushindi wa kutupa mkuki kwa wanaume miaka 60 - 64 kwenye mashindano ya Ulaya mzima katika mji wa Aarhus. 
Amekuwa mshindi wa tatu katika kutupa mkuki kwa wenye umri wa miaka 60 - 64 katika mashindano ya watu kuanzia umri wa miaka 35 kwenda juu kwa nchi zote za Ulaya (European Masters Athletics Championships Stadia).
Michezo hii hufanyika kila baada ya miaka miwili.
Mara ya kwanza na mwisho kushiriki Shururwai Laanyuni ilikuwa mwaka 2004 kwenye mkuki; na kufanikiwa kushika nafasi ya 6.
Mwaka huu amebahatika kupata nafasi ya tatu, na kupata medali ya shaba (bronze).
Kwa ushindi wake huo pia inatufundisha kwamba hata sisi waTanzania tuishio ughaibuni hususani Denmark tunayo nafasi ya kuungana pamoja na kufanya michezo kama familia, kwani michezo ni afya na pia hukutanisha wana jamii ya watanzania na wazawa wa hapa Denmark. Source www.tanden.dk

Miss Tanzania wa Kwanza

MISS TANZANIA 1967-THERESA SHAYO

Mrembo wa kwanza kunyakua taji la Miss Tanzania 1967 shindano lililofanyika hoteli ya Kilimanjaro

Hakufanikiwa kuwania taji la mrembo wa dunia kutokana na serikali ya Tanzania kuyapiga marufuku mashindano hayo kutokana na maadili ya kitanzania.

Aliolewa na mjerumani Chrisian Rieger lakini hakufanikiwa kupata mtoto.

 

Alifariki dunia mwaka 2007 akiwa na umri wa miaka 61 nchini Augsburg Ujerumani kwa maradhi ya kansa ya tumbo na alizikwa huko huko.

Visitors Counter

027835
Today
Yesterday
This Week
Last Week
This Month
Last Month
All days
53
129
657
26031
4725
4022
27835
Your IP: 50.19.34.255
2018-02-24 14:23

The Lastest posts

Contact Us

  • Tanzania Book of Records
  • Sinza Mori, T-Garden street,
  • House No 13
  • P.O.BOX 62279 Dar es salaam
  • 0737208872

       > Site Administrator

Our Facebook Page